Neno Laonekana katika Mwili, Gombo la 7. Kuhusu Ufuatiliaji wa Ukweli lina ushirika na mahubiri maalum ya Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, kwa makanisa. Mahubiri haya na ushirika huu vinaeleza kwa uwazi na dhahiri inamaanisha nini kuufuatilia ukweli, na umuhimu wa kuufuatilia ukweli ni nini, vikifunua uelewa usio sahihi na ufahamu potofu mbalimbali wa mwanadamu kuhusu ufuatiliaji wa ukweli, na vilevile fikira na mitazamo mbalimbali yenye makosa, na dhana na mawazo ya kufikirika ya mwanadamu, huku pia vikivichanganua na vikivitambua. Zaidi ya hayo, mahubiri haya na ushirika huu vinamwonyesha mwanadamu njia za kuufuatilia ukweli na kuingia katika uhalisi. Ukweli huu ni wa umuhimu mkubwa kwa watu wanaoufuatilia ukweli ili wafikie wokovu.
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho