Sura ya 15

Kuonekana kwa Mungu tayari kumetukia katika makanisa yote. Ni Roho ndiye anayenena; Yeye ni moto uwakao kwa ukali, ana uadhama, na anahukumu. Yeye ni Mwana wa Adamu, aliyevikwa vazi linaloshuka hadi miguuni Pake, na mshipi wa dhahabu umefungwa kifuani Pake. Kichwa Chake na nywele Zake ni nyeupe kama sufu, na macho Yake ni kama miali ya moto; miguu Yake ni sawa na shaba nzuri, kana kwamba imesafishwa katika tanuu, na sauti Yake ni kama sauti ya maji mengi. Anashikilia katika mkono Wake wa kuume nyota saba na kinywani Mwake mna upanga mkali wenye makali kuwili, na uso Wake unang'aa kwa ukali kama jua linalowaka!

Mwana wa Adamu ameshuhudiwa, na Mungu Mwenyewe amefunuliwa waziwazi. Utukufu wa Mungu umetoka, uking'aa kwa ukali kama jua linalochoma! Uso Wake mtukufu unang’aa kwa mwanga unaong'aa sana; ni macho ya nani yanayothubutu kumchukulia kwa upinzani? Upinzani husababisha kifo! Hakuna huruma hata kidogo inayoonyeshwa kwa chochote mnachofikiria mioyoni mwenu, neno lolote mnalotamka, au chochote mnachofanya. Ninyi nyote mtakuja kuelewa na kuona kile ambacho mmepata—si kingine ila hukumu Yangu! Je, Ninaweza kuvumilia wakati ninyi hamtii bidii yenu katika kula na kunywa maneno Yangu, na badala yake mnavuruga kiholela na kuharibu ujenzi Wangu? Sitamtendea mtu wa aina hii kwa upole! Tabia yako ikizorota kwa uzito zaidi, utateketezwa katika miali ya moto! Mwenyezi Mungu anajidhihirisha katika mwili wa kiroho, bila hata chembe ya nyama au damu inayounganisha wayoni hadi utosini. Yeye anapita ulimwengu dunia, akiwa ameketi kwenye kiti kitukufu cha enzi katika mbingu ya tatu, akitawala juu ya vitu vyote! Ulimwengu na vitu vyote viko mikononi Mwangu. Ninanena, na yanafanyika. Ninaamuru, na inaamuriwa hivyo. Shetani yuko chini ya miguu Yangu; yuko katika shimo lisilo na mwisho! Sauti Yangu inapotoka, mbingu na ardhi zitapita na zinaisha! Vitu vyote vitafanywa upya; huu ni ukweli usiobadilika milele ambao ni sahihi kabisa. Nimeishinda dunia, pamoja na waovu wote. Nimeketi hapa Nikizungumza nanyi, na wote walio na masikio wanapaswa kusikiliza na wote walio hai wanapaswa kukubali.

Siku zitafikia mwisho; vitu vyote katika dunia hii vitaisha, na vitu vyote vitazaliwa upya. Kumbukeni hili! Kumbukeni! Hamwezi kuwa wazembe kuhusu hili. Mbingu na ardhi zitapita, lakini maneno Yangu hayatapita! Acha Niwahimize kwa mara nyingine tena: Msikimbie bure! Amkeni! Geukeni, na ufuo uko karibu! Tayari Nimeonekana miongoni mwenu, na sauti Yangu imeinuka. Sauti Yangu imeinuka mbele yenu; kila siku inawakabili, uso kwa uso, na kila siku ni mpya na yenye uzima. Wewe unaniona na Mimi ninakuona; Ninazungumza na wewe kila mara, na Niko uso kwa uso na wewe. Hata hivyo, wewe unanikataa na hunijui. Kondoo Wangu wanaweza kuisikia sauti Yangu, lakini bado ninyi mnasita! Mnasita! Moyo wenu umekuwa mzito, macho yenu yamepofushwa na Shetani, na hamwezi kuuona uso Wangu mtukufu—jinsi gani mlivyo wa kusikitisha! Mnasikitisha jinsi gani!

Roho saba walio mbele ya kiti Changu cha enzi wametumwa katika pembe zote za dunia na Nitamtuma Mjumbe Wangu anene na makanisa. Mimi ni mwenye haki na mwaminifu; Mimi ni Mungu anayechunguza sehemu za ndani kabisa za moyo wa mwanadamu. Roho Mtakatifu ananena na makanisa, na ni maneno Yangu yanayotoka ndani ya Mwana Wangu. Wale wote walio na masikio wanapaswa kusikiliza! Wale wote walio hai wanapaswa kukubali! Yaleni na yanyweni tu, na msishuku. Wale wote wanaotii na kuyasikiliza maneno Yangu watapokea baraka kuu! Wale wote wanaotafuta uso Wangu kwa dhati hakika watakuwa na mwanga mpya, nuru mpya, na umaizi mpya; yote yatakuwa mapya na ya sasa. Maneno Yangu yatakuonekania wakati wowote, na yatafungua macho yako ya kiroho ili uweze kuona siri zote za ulimwengu wa kiroho. Ufalme uko miongoni mwa wanadamu. Ingia katika kimbilio, na neema na baraka zote zitakuwa juu yako; njaa na tauni hazitaweza kukukaribia, na mbwa mwitu, nyoka, simbamarara, na chui hawataweza kukudhuru. Wewe utaenda na Mimi, utatembea na Mimi, na utaingia katika utukufu na Mimi!

Mwenyezi Mungu! Amefunua waziwazi mwili Wake mtukufu, mwili Wake mtakatifu wa kiroho umeonekana, na Yeye ni Mungu mkamilifu Mwenyewe! Dunia na mwili Wake vyote vimebadilishwa, na kugeuka sura Kwake mlimani ni nafsi ya Mungu. Anavaa taji la dhahabu kichwani Pake, mavazi Yake ni meupe pe, kifuani Pake kuna mshipi wa dhahabu, na dunia na vitu vyote ni kibao cha kuwekea miguu Yake. Macho Yake ni kama miali ya moto, kinywani Mwake mna upanga mkali wenye makali kuwili, na Anashikilia nyota saba katika mkono Wake wa kuume. Njia ya ufalme inang'aa bila kikomo, na mwanga Wake mtukufu unainuka na kung'aa; milima inafurahi na maji yanacheka, na jua, mwezi, na nyota vyote vinazunguka katika mpangilio wao wa utaratibu, vikikaribisha kurudi kwa ushindi kwa Mungu mmoja wa kweli ambaye amekamilisha mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita. Wote wanaruka na kucheza kwa furaha! Furahini! Mwenyezi Mungu ameketi kwenye kiti Chake kitukufu cha enzi! Imbeni! Bendera ya ushindi ya Mwenyezi imeinuliwa juu kwenye Mlima Sayuni wenye uadhama na utukufu! Kila taifa linafurahi, watu wateule wa Mungu wasiohesabika wanaimba, Mlima Sayuni unacheka kwa furaha, na utukufu wa Mungu umeinuka! Sikuwahi hata kuota kwamba ningeuona uso wa Mungu, lakini leo nimeuona. Nikiwa uso kwa uso na Yeye kila siku, ninazungumza na Yeye na kuuweka wazi moyo wangu. Yeye anaruzuku chakula na kinywaji kwa wingi. Katika maisha, maneno, matendo, mawazo, na fikira, mwanga Wake mtukufu unaangaza, Yeye anaongoza kila hatua ya njia, na mtu akiasi moyoni, hukumu Yake inashuka haraka.

Kula, kukaa, na kuishi pamoja na Mungu, kuwa pamoja na Yeye, kutembea pamoja, kufurahia pamoja, kupata utukufu na baraka pamoja, kutawala kama wafalme pamoja na Mungu, na kuwa pamoja katika ufalme—ni raha iliyoje! Ni tamu jinsi gani! Tuko uso kwa uso na Yeye kila siku, Yeye ananena kila siku na kuzungumza nasi kila mara, na tunajaliwa nuru mpya na umaizi mpya kila siku. Macho yetu ya kiroho yakiwa yamefunguliwa, tunaona kila kitu; siri za roho zinafunuliwa kwetu. Maisha matakatifu kwa kweli ni changamfu; kimbieni haraka na msisimame, na msonge mbele bila kukoma—kuna maisha ya ajabu zaidi mbele. Msiridhike na kuonja utamu tu; kimbieni mpaka mwisho ndani ya Mungu. Yeye anajumuisha yote na ni mkarimu, na ana vitu vya kila aina ambavyo tunakosa. Shirikianeni kwa bidii na mwingie ndani Yake, na kila kitu kitabadilika. Maisha yetu yatazidi uwezo wa binadamu, na hakuna mtu, tukio, au kitu kitakachoweza kutusumbua.

Kuzidi uwezo wa binadamu! Kuzidi uwezo wa binadamu! Kuzidi uwezo wa binadamu kweli! Maisha ya Mungu yazidiyo uwezo wa binadamu yako ndani, na vitu vyote vimekuwa tulivu kweli! Tunaenda zaidi ya dunia na vitu vya kidunia, hatuhisi uambatisho wowote kwa waume au watoto. Tunazidi vizuizi vya ugonjwa na mazingira. Shetani hathubutu kutusumbua. Tunazidi kabisa maafa yote. Huku ni kumruhusu Mungu kuchukua ufalme! Tunamkanyaga Shetani chini ya miguu, tunasimama kwa uthabiti katika ushuhuda wetu kwa ajili ya kanisa, na tunafichua kikamilifu sura mbaya ya Shetani. Ujenzi wa kanisa uko ndani ya Kristo, na mwili mtukufu umeinuka—huku ni kuishi katika hali ya kunyakuliwa!

Iliyotangulia:  Sura ya 14

Inayofuata:  Sura ya 16

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Connect with us on Messenger