Mungu Anashikilia Mamlaka Juu ya Hatima ya Binadamu Wote
Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo waaminifu, ni jukumu na wajibu wetu sote kutoa akili zetu na miili yetu kwa ajili ya kutimiza agizo la Mungu, kwa maana nafsi yetu yote inatoka kwa Mungu, na tunaishi kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Kama akili na miili yetu haijatolewa kwa ajili ya agizo la Mungu na kusudi la haki ya binadamu, basi roho zetu zitahisi aibu mbele ya wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na zaidi sana zitahisi aibu mbele ya Mungu, aliyetupa kila kitu.
Mungu aliumba ulimwengu huu, Alimuumba binadamu huyu na, zaidi ya hayo, Alikuwa muasisi wa utamaduni wa kale wa Kigiriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu pekee Anayewaliwaza wanadamu hawa, na ni Mungu pekee Anayewalinda binadamu hawa usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatenganishwi na mamlaka ya Mungu, na historia na mustakabali wa binadamu hauwezi kuepuka mipango inayofanywa na mikono ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi kwa hakika utaamini kwamba kuinuka na kuanguka kwa nchi ama taifa lolote kuko chini ya mipango ya Mungu. Mungu pekee ndiye Anayejua hatima ya nchi ama taifa lolote, na ni Mungu pekee ndiye Anayedhibiti mwenendo wa binadamu hawa. Ikiwa wanadamu wanataka kuwa na hatima nzuri, ikiwa nchi inataka kuwa na hatima nzuri, basi wote lazima wasujudu na wamwabudu Yeye, na waje mbele ya Mungu kutubu na kuungama Kwake, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu yatakuwa janga lisiloepukika.
Angalia nyuma wakati Nuhu alipojenga safina: Binadamu walikuwa wamepotoka sana, na walikuwa wamepotea kutoka katika baraka za Mungu, hawakuwa wanalindwa na Mungu tena, na walikuwa wamepoteza ahadi za Mungu. Waliishi gizani, bila mwangaza wa Mungu. Kisha wakawa waasherati kiasili, na wakapotoka kwa kiwango cha kuchukiza. Watu kama hao hawangeweza tena kupokea ahadi za Mungu; hawakufaa kushuhudia uso wa Mungu, wala kuisikia sauti ya Mungu, kwani walikuwa wamemwacha Mungu, waliweka kando yote Aliyowakirimu, na walikuwa wamesahau maneno ya Mungu ya mafundisho. Mioyo yao ilienda mbali zaidi na zaidi kutoka kwa Mungu, na baadaye, wakawa wapotovu kufikia kiasi kwamba walipoteza busara na ubinadamu wote, na wakazidi kuwa waovu. Kisha walitembea kuelekea kifo na wakaanguka chini ya ghadhabu na adhabu ya Mungu. Ni Nuhu tu aliyemwabudu Mungu na kuepukana na uovu, na hivyo aliweza kuisikia sauti ya Mungu na kusikia maagizo Yake. Alijenga safina kulingana na maagizo ya neno la Mungu, na hapo akakusanya aina zote za viumbe hai. Na kwa njia hii, wakati kila kitu kilikuwa kimetayarishwa, Mungu alianza kazi Yake ya kuiangamiza dunia. Ni Nuhu tu na watu saba wa familia yake walionusurika maangamizi, kwani Nuhu alimwabudu Yehova na kuepuka maovu.
Sasa tazama enzi ya sasa: Watu wenye haki kama Nuhu, ambao waliweza kumwabudu Mungu na kuepuka maovu, wamekoma kuwepo. Hata hivyo Mungu bado anawafadhili binadamu hawa na bado Anawaonyesha binadamu wa enzi hii ya mwisho msamaha. Mungu anawatafuta wale wanaotamani sana kuonekana Kwake, anawatafuta wale wanaosikiliza maneno Yake, anawatafuta wale wasiosahau agizo Lake na wanaomtolea Yeye mioyo na miili yao, na anawatafuta wale ambao ni watiifu na wasiopinga kama watoto wachanga mbele Yake. Ikiwa utajitoa kwa Mungu, bila kuzuiliwa na nguvu yoyote, basi Mungu atakutazama kwa upendeleo na atakukirimia baraka Zake. Ikiwa una hadhi ya juu, sifa kuu, maarifa mengi, mali nyingi, na uungwaji mkono wa watu wengi, lakini unabaki bila kuhangaishwa na mambo haya na bado unakuja mbele ya Mungu kukubali wito Wake na agizo Lake na kufanya kile ambacho Mungu anakwambia ufanye, basi yote unayofanya yatakuwa kazi ya maana zaidi duniani na kazi ya haki zaidi ya binadamu. Ukikataa wito wa Mungu kwa ajili ya hadhi au malengo yako mwenyewe, yote unayofanya yatalaaniwa na, zaidi ya hayo, yatachukiwa na Mungu. Pengine wewe ni rais, mwanasayansi, mchungaji, au mzee, lakini haijalishi cheo chako ni cha juu kiasi gani, ikiwa unatumia uwezo wako na maarifa yako kutekeleza kazi yako mwenyewe, basi utakuwa mtu aliyeshindwa daima na utakuwa daima umekosa baraka za Mungu, kwa sababu Mungu hakubali chochote unachofanya, na Yeye hakubali kwamba kazi yako ni ya haki, wala hatambui kwamba unafanya kazi kwa ajili ya manufaa ya wanadamu. Atasema kwamba kila kitu unachofanya ni kutumia maarifa na nguvu za binadamu kujaribu kusukuma mbali ulinzi wa Mungu kwa mwanadamu, na kwamba ni kukanusha baraka za Mungu. Yeye atasema kwamba unawaongoza wanadamu kuelekea gizani, kuelekea kifo, na kuelekea mwanzo wa uwepo usio na mipaka ambapo mwanadamu hana Mungu na amepoteza baraka Zake.
Tangu ujio wa sayansi ya kijamii, moyo wa mwanadamu umechukuliwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa zimekuwa zana za kuwatawala wanadamu, zikimwacha mwanadamu bila nafasi ya kutosha kumwabudu Mungu, na bila hali nyingi sana zinazofaa za kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu imeendelea kushuka chini zaidi na zaidi moyoni mwa mwanadamu. Bila nafasi ya Mungu mioyoni mwake, ulimwengu wa ndani wa mwanadamu ni wa giza, usio na tumaini na ni mtupu. Kisha wanasayansi wengi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi wamekuja katika mstari wa mbele kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia nyingine zinazopinga ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, ili kujaza mioyo na akili za wanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wamekuwa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wameendelea kuwa wengi zaidi na zaidi kwa idadi. Watu zaidi na zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa enzi ya Agano la Kale kuwa hadithi na hekaya. Mioyoni mwao, watu wanakuwa wasiojali hadhi na ukuu wa Mungu, na wanakuwa wasiojali kuhusu uwepo wa Mungu na imani kwamba Mungu anatawala juu ya vitu vyote. Kuendelea kuishi kwa wanadamu na hatima ya nchi na mataifa si muhimu tena kwao, na mwanadamu anaishi katika ulimwengu ulio mtupu unaojishughulisha tu na kula, kunywa, na kutafuta raha. … Ni watu wachache wanaojishughulisha kutafuta mahali ambapo Mungu anafanya kazi Yake leo, au kutafuta jinsi Anavyoshikilia mamlaka na kupanga hatima ya mwanadamu. Na kwa njia hii, bila ya mwanadamu kujua, ustaarabu wa mwanadamu unashindwa zaidi na zaidi kuendana na matakwa ya mwanadamu, na hata kuna watu wengi ambao wanahisi kwamba, kuishi katika ulimwengu kama huu, wana furaha kidogo kuliko wale ambao wamekufa tayari. Hata watu wa nchi zilizokuwa na ustaarabu wa hali ya juu wanatoa malalamiko kama hayo. Kwani bila mwongozo wa Mungu, hata watawala na wanasosholojia wakipiga bongo zao ili kuhifadhi ustaarabu wa mwanadamu, haitakuwa na mafanikio. Hakuna mtu anayeweza kujaza utupu ulio moyoni mwa mwanadamu, kwani hakuna mtu anayeweza kuwa uzima wa mwanadamu, na hakuna nadharia ya kijamii inayoweza kumweka huru mwanadamu kutokana na matatizo ya utupu. Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, furaha na faraja humletea mwanadamu maliwazo ya muda tu. Hata kukiwa na mambo haya, mwanadamu bado haepuki kutenda dhambi na kulalamika kuhusu ukosefu wa haki katika jamii. Kuwa na mambo haya hakuwezi kuzuia kutamani sana na hamu ya mwanadamu ya kuchunguza. Hii ni kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu na kujitoa kwake na uchunguzi usio na maana unaweza tu kuzidi kumletea dhiki, na kumfanya mwanadamu awe katika hali ya wasiwasi ya siku zote, asijue jinsi ya kuukabili mustakabali wa wanadamu au jinsi ya kuikabili njia iliyo mbele, hadi kufikia kiwango ambapo mwanadamu hata anaogopa sayansi na maarifa, na hata zaidi anahofia hisia ya utupu iliyo ndani yake. Katika ulimwengu huu, bila kujali kama unaishi katika nchi huru ama isiyo na haki za binadamu, huwezi kabisa kuponyoka majaliwa ya mwanadamu. Kama wewe ni kiongozi ama anayeongozwa, huwezi kabisa kuponyoka hamu ya kuchunguza majaliwa, mafumbo, na hatima ya wanadamu, sembuse kuweza kutoroka hisia ya utupu isiyoelezeka. Matukio kama haya, yaliyo kawaida kwa wanadamu wote, yanaitwa matukio ya kijamii na wanasosholojia, lakini hakuna mtu mkuu anayeweza kuja kutatua shida kama hizi. Mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu, na hadhi na uzima wa Mungu haviwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Kile ambacho mwanadamu anahitaji si tu jamii iliyo na haki, ambapo kila mtu analishwa vyema, yenye usawa, na huru; kile ambacho mwanadamu anahitaji ni wokovu wa Mungu na utoaji Wake wa uzima kwa mwanadamu. Ni pale tu ambapo mwanadamu anapopokea utoaji wa Mungu wa uzima na wokovu Wake ndipo mahitaji yake, matamanio yake ya kuchunguza, na utupu ulio moyoni mwake utaweza kutatuliwa. Ikiwa watu wa nchi ama taifa fulani hawawezi kupokea wokovu na ulinzi wa Mungu, basi nchi ama taifa kama hilo litaelekea kuanguka, kuelekea gizani, na kama matokeo litaangamizwa na Mungu.
Pengine nchi yako inaendelea kwa sasa, lakini ukiruhusu watu wako waende mbali na Mungu, basi nchi yako itazidi kujipata bila baraka za Mungu, ustaarabu wake utazidi kukanyagiwa chini ya mguu wa mwanadamu, na, kabla ya muda mrefu, watu wake watainuka kumpinga Mungu na kuilaani Mbingu. Kwa njia hii, bila kujua, hatima ya nchi itaharibiwa. Mungu ataziinua nchi zenye nguvu ili kukabiliana na nchi hizo zilizolaaniwa na Mungu, na Anaweza hata kuziangamiza kutoka kwenye uso wa dunia. Jambo la msingi katika usitawi au kuangamia kwa nchi ama taifa ni kama watawala wake wanamwabudu Mungu, na kama wanawaongoza watu wake kumkaribia Mungu na kumwabudu. Lakini katika enzi hii ya mwisho, kwa sababu wale wanaomtafuta na kumwabudu Mungu kwa dhati wanazidi kuwa wachache, Mungu anatoa upendeleo wa pekee kwa nchi ambazo Ukristo ni dini ya taifa. Anazikusanya nchi hizo pamoja ili kuunda kambi ya ulimwengu yenye haki kwa ulinganisho, huku nchi zinazomkana Mungu na zile nchi zisizomwabudu Mungu wa kweli zinakuwa wapinzani wa kambi hiyo ya haki. Kwa njia hii, Mungu hana tu nafasi miongoni mwa wanadamu ambapo Anaweza kufanyia kazi Yake, lakini pia wakati huo huo, Anapata nchi zinazoweza kutumia mamlaka ya haki, Akiruhusu vizuizi na vikwazo kuwekwa juu ya nchi hizo zinazompinga. Licha ya hayo, Mungu bado hawezi kuwapata watu zaidi wa kumwabudu, kwa sababu mwanadamu amepotea mbali sana kutoka Kwake, na amemsahau Mungu kwa muda mrefu sana, na katika dunia hii kumebaki tu nchi ambazo zinatenda haki na kupinga udhalimu. Lakini hii ipo mbali na kufikia matarajio ya Mungu, kwa kuwa hakuna watawala wa nchi watakaomruhusu Mungu awatawale watu wao, na hakuna chama cha kisiasa cha nchi kitakachowakusanya pamoja watu wake ili wampe Mungu heshima kuu; Mungu amepoteza nafasi Yake inayostahili katika moyo wa kila nchi, taifa, chama tawala, na hata katika moyo wa kila mtu. Ingawa baadhi ya nguvu za haki zipo katika ulimwengu huu, utawala wowote ambao kwao Mungu hana nafasi ndani ya moyo wa mwanadamu ni dhaifu sana, na uwanja wa kisiasa, ambao hauna baraka za Mungu, upo katika mkanganyiko na hauwezi kustahimili hata pigo moja. Kwa wanadamu, kutokuwa na baraka za Mungu ni sawa na kutokuwa na jua. Bila kujali jinsi watawala wanavyotoa michango kwa uangalifu kwa watu wao, bila kujali ni mikutano mingapi ya haki ambayo wanadamu wanafanya pamoja, hakuna hata moja kati ya haya litakaloweza kugeuza wimbi hilo au kubadilisha hatima ya wanadamu. Mwanadamu anaamini kwamba nchi ambayo watu wanalishwa na kuvishwa, ambayo watu wanaishi pamoja kwa amani, ndiyo nchi nzuri, na yenye uongozi mzuri. Lakini Mungu hafikirii hivyo. Anaamini kuwa nchi ambayo hakuna mtu anayemwabudu ndiyo Atakayoiangamiza. Mawazo ya mwanadamu hutofautiana kabisa na ya Mungu. Kwa hivyo, kama mkuu wa nchi hamwabudu Mungu, basi majaliwa ya nchi hii yatakuwa ya tanzia, na nchi hii haitakuwa na hatima.
Mungu hashiriki katika siasa za mwanadamu, lakini Anadhibiti majaliwa ya kila nchi na taifa, Anadhibiti dunia hii na ulimwengu mzima. Majaliwa ya binadamu na mpango wa Mungu vimeunganishwa kwa karibu, na hakuna mtu, nchi, au taifa linaloweza kuepuka mamlaka ya Mungu. Mwanadamu akitamani kujua hatima yake, basi lazima aje mbele za Mungu. Mungu atawafanya wanaomfuata na kumwabudu kufanikiwa na Atawashusha na kuwaangamiza wale wanaompinga na kumkataa.
Kumbuka tukio katika Biblia ambapo Mungu aliangamiza Sodoma, na fikiria pia jinsi mke wa Lutu alivyokuwa nguzo ya chumvi. Kumbuka jinsi watu wa Ninawi walivyotubu na kuungama dhambi zao wakiwa kwenye magunia na majivu. Kumbuka Wayahudi walifikia mwisho upi baada ya kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita—walifukuzwa kutoka Israeli na kukimbilia nchi za ulimwengu, wengi waliuawa, na taifa zima la Kiyahudi lilipatwa na uchungu usio na kifani wa kuangamizwa kwa nchi yao. Walikuwa wamempigilia Mungu msalabani—walitenda dhambi ya kutisha—na wakaichokoza tabia ya Mungu. Walilazimika kulipia kile walichotenda na walilazimika kubeba matokeo yote ya vitendo vyao. Walimhukumu Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na hatima moja tu: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo yalikuwa matokeo machungu na maafa ambayo watawala wao walileta juu ya nchi na taifa lao.
Leo, Mungu amerudi miongoni mwa watu kufanya kazi Yake na kituo Chake cha kwanza katika kazi Yake ni kielelezo kikuu cha udikteta: Uchina, ngome thabiti ya ukanaji Mungu. Mungu amelipata kundi la watu kwa hekima na nguvu Zake. Katika wakati huu, Amewindwa na chama tawala cha Uchina kwa kila namna na kukabiliwa na mateso ya kila aina, bila mahala pa kupumzisha kichwa Chake na bila mahali pa kujikinga. Licha ya haya, Mungu bado anaendelea kufanya kazi Aliyonuia kufanya: Ananena na kutamka maneno, na Anaeneza injili. Hakuna mtu anayeweza kuelewa uweza wa Mungu. Huko Uchina, nchi inayomchukulia Mungu kama adui, Mungu hajawahi kukoma kazi Yake. Badala yake, watu wengi zaidi wamekubali kazi na neno Lake, kwani Mungu humwokoa kila mwanadamu mmoja mmoja kwa kiwango kikubwa iwezekanavyo. Sote tunaamini kwamba hakuna nchi au nguvu inayoweza kuzuia kile ambacho Mungu ananuia kutimiza, na kwamba wale wanaojaribu kuizuia kazi ya Mungu, wale wanaopinga neno la Mungu, na wale wanaovuruga na kujaribu kuharibu mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Mtu yeyote anayepinga kazi ya Mungu atafukuzwa kwenda kuzimu na Mungu; nchi yoyote inayoipinga kazi ya Mungu itaangamizwa na Mungu; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka kwenye dunia hii na Mungu na litakoma kuwepo. Ninawahimiza watu wa mataifa yote na wa nchi zote, na hata wa tasnia zote waje waisikilize sauti ya Mungu, waje waitazame kazi ya Mungu na wazingatie hatima ya binadamu, na hivyo wamfanye Mungu kuwa ndiye mtakatifu zaidi, mwenye kuheshimiwa zaidi, mkuu zaidi, na wa pekee wa kuabudiwa miongoni mwa binadamu, na kuwawezesha binadamu wote waishi katikati ya baraka za Mungu, kama tu vile uzao wa Ibrahimu walivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu vile Adamu na Hawa, ambao Mungu aliwaumba hapo mwanzo, walivyoishi katika Bustani ya Edeni.
Kazi ya Mungu inasonga mbele kama wimbi kuu lenye nguvu. Hakuna anayeweza kumzuia, na hakuna anayeweza kusimamisha hatua Zake. Ni wale tu wanaosikiliza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kumwonea kiu, ndio wanaoweza kufuata hatua Zake na kupokea ahadi Yake. Wale wasiofanya hivyo watakabiliwa na janga la kuangamiza na adhabu wanayostahili kabisa.