154  Kupitia Katika Upepo na Mvua

1

Ee Mungu! Nimekupa moyo wangu. Mungu wa vitendo, Wewe wapendeza sana.

Umejinyenyekeza katika mwili, Ukitembea kati yetu.

Umeonyesha ukweli ili kuwaokoa wanadamu, Ukitulisha , kututunza, na kutunyunyizia kwa uvumilivu.

Unavumilia kukataliwa na kukashifiwa kwa kimya, mfano kwa mwanadamu kila mahali.

Kwa uongozi Wako moyo wangu unaridhika, maneno Yako yanaiangaza njia iliyo mbele.

Nafuata kwa karibu katika nyayo Zako, naomba nipite katika upepo na mvua yote pamoja na Wewe.

2

Ee Mungu! Nimekupa moyo wangu. Mungu wa vitendo, Wewe wapendeza sana.

Hukumu na kuadibu Kwako vinafichua upendo Wako wote.

Tunatakaswa na Wewe, tunafanywa upya na kubadilishwa, tunakuwa wanadamu wapya.

Haki na utakatifu Wako ni vya kupendeza sana, Unautawala moyo wangu kikamilifu.

Maneno Yako yametukamilisha, tuko moyo mmoja na Wewe, tunakua karibu sana na Wewe.

Nafuata kwa karibu katika nyayo Zako, naomba nipite katika upepo na mvua yote pamoja na Wewe.

3

Ee Mungu! Nimekupa moyo wangu. Mungu wa vitendo, Wewe wapendeza sana.

Ingawa tumeteseka sana kupitia ugumu na mateso, upendo Wako pamoja na maneno Yako hutuongoza,

ili tuwe na imani na nguvu na kukushuhudia Wewe katika shida.

Tutakupenda daima na kulipa upendo Wako, tutaeneza ukweli na kukushuhudia.

Miaka ya umoja na upendo wa pande zote, upendo wetu umeongezeka kupitia upepo mkali na mvua nzito.

Nafuata kwa karibu katika nyayo Zako, naomba nipite katika upepo na mvua yote pamoja na Wewe.

Iliyotangulia:  151  Siwezi Kusema Yote Yaliyo Moyoni Mwangu

Inayofuata:  157  Ni Vizuri Sana Kwamba Mwenyezi Mungu Amekuja

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Connect with us on Messenger