Juu ya Hatima

Wakati wowote hatima inatajwa, mnaichukulia kwa uzito maalum; nyote ni wasikivu haswa kuhusiana na jambo hili. Baadhi ya watu hawawezi kusubiri kumsujudia Mungu ili hatimaye waweze kuwa na hatima nzuri. Naweza kutambua shauku yenu, ambayo haihitaji kuonyeshwa katika maneno. Hamtaki kabisa miili yenu ianguke katika maafa, na hata zaidi, hamtaki kushuka katika adhabu ya muda mrefu hapo baadaye. Mnatarajia tu kujiruhusu muishi kwa uhuru zaidi kidogo, kwa urahisi zaidi kidogo. Na hivyo unahisi wasiwasi hasa kila wakati ambapo hatima inatajwa, unahofia sana kwamba, usipokuwa mwangalifu vya kutosha, unaweza kumkosea Mungu na hivyo utapata adhabu unayostahili. Hamjasita kufanya maafikiano kwa ajili ya hatima zenu, na wengi wenu ambao hapo awali mlikuwa wapotovu na wazembe hata ghafla mmegeuka hasa wapole na wakweli; uaminifu wenu hata una mzizimo. Bila kujali, nyote mna mioyo ya uaminifu, na tangu mwanzo hadi mwisho mmejifungua wazi Kwangu bila kuficha siri zozote ndani ya mioyo yenu, ziwe lawama, udanganyifu, au kujitolea. Kwa ujumla, “mmekiri” kwa uwazi Kwangu mambo muhimu yaliyopo katika mahali pa siri pa nafsi zenu. Bila shaka, Sijawahi kuacha kunena moja kwa moja kuhusu mambo kama haya, kwa kuwa yote yanafahamika sana Kwangu. Ni afadhali muingie katika bahari ya moto kwa ajili ya hatima zenu za mwisho, kuliko kupoteza unywele mmoja kwa ajili ya kupata kibali cha Mungu. Sio kwamba Ninakuwa nawalazimisha; ni kwamba mmepungukiwa sana na moyo wa kujitoa katika kukabiliana na kila kitu Ninachofanya. Hamuwezi kuelewa Ninachomaanisha, hivyo basi acheni Niwape maelezo rahisi: Kile mnachohitaji si ukweli na uzima; si kanuni za jinsi ya kutenda, na hasa siyo kazi Yangu yenye kujitahidi. Yote mnayohitaji ni yale ambayo mnamiliki katika mwili—mali, hadhi, familia, ndoa, na kadhalika. Ninyi mnatupilia mbali kabisa maneno na kazi Yangu, hivyo Naweza kujumlisha imani yako kwa neno moja: shingo upande. Mtafanya lolote ili kutimiza mambo ambayo bila shaka mmejitolea, lakini Nimegundua kwamba hampuuzi kila kitu kwa ajili ya mambo ya imani yenu katika Mungu. Badala yake, nyinyi ni waaminifu tu kiasi, na mna bidii kiasi. Ndiyo maana Ninasema kwamba wale ambao hawana moyo wa unyofu kabisa ni wale walioshindwa katika imani yao kwa Mungu. Fikiria kwa makini—je, kuna wengi walioshindwa miongoni mwenu?

Mnapaswa kujua kwamba mafanikio katika kumwamini Mungu yanatimizwa kwa sababu ya matendo ya watu wenyewe; wakati watu hawafanikiwi lakini badala yake wanashindwa, hiyo pia ni kwa sababu ya matendo yao wenyewe, sio matokeo ya vipengele vingine. Ninaamini kwamba mngefanya kitu chochote kinachohitajika ili kupata kitu ambacho ni kigumu zaidi na kinachohitaji mateso zaidi kuliko kumwamini Mungu, na kwamba mngekichukulia kwa umakini sana. Hamngetaka hata kufanya makosa yoyote; hizi ni aina za juhudi za kudumu ambazo nyote mmeweka katika maisha yenu wenyewe. Nyinyi hata mna uwezo wa kunidanganya Mimi katika mwili chini ya hali ambazo hamuwezi kumdanganya yeyote wa familia zenu wenyewe. Hii ni tabia yenu thabiti na kanuni ambayo mnatumia katika maisha yenu. Je, si bado mnaendeleza picha ya uongo ili kunidanganya Mimi, kwa ajili ya hatima zenu, na kuwa na hatima nzuri na yenye furaha? Nafahamu kwamba kujitoa kwenu na unyofu wenu ni wa muda tu; je, matamanio yenu na gharama mnayolipa ni ya sasa tu na si ya baadaye? Mnataka tu kutumia nguvu moja ya mwisho ili kupata hatima nzuri. Kusudi lenu ni kufanya mabadilishano tu; siyo ili msiwe wenye deni kwa ukweli, na ni hasa msinilipe kwa ajili ya gharama Niliyolipa. Kwa neno moja, mko tayari kutumia ujanja wenu tu, lakini hamko tayari kuipigania. Je, hii si nia yenu ya dhati? Sio lazima mjifiche, na hata zaidi, sio lazima mpige bongo zenu juu ya hatima zenu hadi pale ambapo hamuwezi kula au kulala. Je, si ni kweli kwamba matokeo yenu yatakuwa yameamuliwa mwishowe? Mnapaswa kufanya wajibu wenu wenyewe kwa kadri ya uwezo wenu kwa mioyo iliyo wazi na yenye uaminifu, na muwe tayari kufanya chochote kitakachohitajika. Kama mlivyosema, siku itakapowadia, Mungu hatakosa kumjali mtu yeyote ambaye aliteseka au kulipa gharama kwa ajili Yake. Aina hii ya imani ni yenye thamani kuishikilia, na hampaswi kuisahau kamwe. Ni kwa njia hii tu Ninaweza kutuliza akili Yangu kuwahusu. Vinginevyo, Sitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu, na milele mtakuwa walengwa wa chuki Yangu. Kama nyote mnaweza kufuata dhamiri zenu na kutoa yote kwa ajili Yangu, mkitoa juhudi zote kwa ajili ya kazi Yangu, na kutoa juhudi za maisha yote kwa ajili ya kazi ya injili Yangu, basi si moyo Wangu mara kwa mara utaruka kwa furaha kwa ajili yenu? Si Mimi Nitakuwa na uwezo wa kutuliza akili Yangu kuwahusu? Ni aibu kwamba kile mnachoweza kufanya ni cha kusikitisha sana, na ni sehemu ndogo sana ya kile Ninachotarajia; kwa hali hii, mnawezaje kuwa na ujasiri wa kutafuta kutoka Kwangu kile mnachotumainia?

Hatima zenu na majaliwa yenu ni muhimu sana kwenu—zina umuhimu mkubwa sana. Mnaamini kuwa msipofanya mambo kwa uangalifu sana, itakuwa sawa na kutokuwa na hatima, na uharibifu wa majaliwa yenu. Lakini mmewahi kufikiri kwamba kama juhudi ambazo mtu anatumia, ni kwa ajili tu ya hatima zao wenyewe, hizo zitakuwa tu ni kazi zisizo na matunda? Juhudi kama hizo si za kweli—ni bandia na danganyifu. Kama ni hivyo, wale ambao wanafanya kazi kwa ajili ya hatima zao watapokea maangamizo yao ya mwisho, kwa sababu kushindwa kwa imani za watu katika Mungu kumesababishwa na udanganyifu. Hapo awali Nilisema kwamba Sipendi kubembelezwa au kusifiwa kinafiki, au kutendewa kwa shauku kubwa. Ninapenda watu waaminifu ili wakabiliane na ukweli na matarajio Yangu. Hata zaidi, Ninapenda wakati watu wanapoweza kuonyesha uangalifu mkubwa na kuujali moyo Wangu, na wakati wanapoweza hata kuacha kila kitu kwa ajili Yangu. Ni kwa njia hii tu ndipo Moyo wangu utaweza kufarijiwa. Kwa sasa, je, kuna mambo mangapi kukuhusu ambayo Siyapendi? Je, kuna mambo mangapi kukuhusu ambayo Nayapenda? Je, inawezekana kwamba hakuna yeyote kati yenu ambaye ametambua ubaya wote ambao mmeonyesha kwa ajili ya hatima zenu?

Katika moyo Wangu, Sitaki kuumiza moyo wowote ambao ni chanya na wenye motisha, na Sitamani hasa kupunguza nguvu ya mtu yeyote ambaye anafanya wajibu wake kwa uaminifu. Hata hivyo, ni lazima Nimkumbushe kila mmoja wenu juu ya upungufu wenu na juu ya nafsi chafu iliyo ndani kabisa ya mioyo yenu. Azma ya kufanya hivyo ni kutarajia kwamba mtaweza kutoa mioyo yenu ya kweli katika kukabiliana na maneno Yangu, kwa sababu kile Ninachochukia zaidi ni udanganyifu wa watu Kwangu. Natarajia tu kuwa katika hatua ya mwisho ya kazi Yangu, mtaweza kutoa utendaji wenu bora zaidi, na kwamba mtajitolea kwa moyo wote, na wala sio shingo upande tena. Bila shaka, Natarajia pia kuwa nyote mtaweza kuwa na hatima nzuri. Hata hivyo, bado Nina mahitaji Yangu ambayo ni kwa nyinyi kufanya uamuzi bora zaidi katika kutoa Kwangu uaminifu wenu wa pekee na wa mwisho. Ikiwa mtu hana huo uaminifu wa pekee, basi kwa hakika mtu huyo atakwenda kuwa hazina ya Shetani, na Sitaendelea tena kumtumia, bali Nitamrudisha nyumbani akatunzwe na wazazi wake. Kazi yangu imekuwa ya msaada sana kwa ajili yenu; kile Ninachotarajia kupata kutoka kwenu ni moyo wenye uaminifu na wenye motisha, lakini mpaka sasa mikono Yangu bado ni mitupu. Fikiria kuhusu hili: Ikiwa siku moja bado Nitakuwa nimekasirika sana, kupita maelezo, je, mtazamo Wangu kwako utakuwaje kwa wakati huo? Je, bado Nitakuwa mwema kwako kwa wakati huo kama Nilivyo sasa? Je, moyo Wangu bado utakuwa mtulivu kwa wakati huo kama ulivyo sasa? Je, mnaelewa hisia za mtu ambaye amelima kwa kujitahidi lakini hakuvuna hata nafaka moja? Je, mnaelewa ukubwa wa jeraha la mtu ambaye amepigwa kipigo kikubwa? Je, mnaweza kuonja uchungu wa mtu aliyejawa na matumaini ambaye anapaswa kuachana na mtu kwa uhusiano mbaya? Je, mmeona hasira ya mtu ambaye amekasirishwa? Je, mnaweza kujua hisia ya kulipiza kisasi kwa haraka ya mtu ambaye amekuwa akichukuliwa kwa uadui na udanganyifu? Kama mnaelewa fikira za watu hawa, Nadhani haiwezi kuwa vigumu kwenu kufikiria mtazamo ambao Mungu Atakuwa nao wakati ule wa adhabu Yake. Hatimaye, Natarajia nyote mtaweka juhudi kubwa kwa ajili ya hatima zenu wenyewe; hata hivyo, ni bora msitumie njia za udanganyifu katika juhudi zenu, ama sivyo Nitasikitishwa nanyi katika moyo Wangu. Je, kusikitishwa kwa aina hii kutasababisha nini? Je, hamjidanganyi wenyewe? Wale ambao wanafikiria juu ya hatima zao lakini bado wanaziharibu ni watu wenye uwezekano mdogo wa kuokolewa. Hata kama watu kama hao watakerwa na kukasirika, ni nani atakayemhurumia mtu kama huyo? Kwa ujumla, bado Ninatamani muwe na hatima inayofaa na nzuri. Hata zaidi, Ninatumai kwamba hakuna yeyote kati yenu atakayeanguka katika maafa.

Iliyotangulia:  Je, Wewe ni Mwaminifu kwa Nani?

Inayofuata:  Maonyo Matatu

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Connect with us on Messenger