Sura ya 71
Mimi Nimejiweka mzima dhahiri kwenu, lakini kwa nini mnashindwa kutafakari maneno Yangu kwa mioyo na nafsi zenu zote? Kwa nini mnayachukulia maneno Yangu kama takataka? Je, Ninayosema si sahihi? Je, maneno Yangu yamewagusa katika sehemu muhimu? Daima kuchelewesha, daima kusita, kwa nini mnafanya mambo hivi? Je, Mimi sijaongea kwa uwazi? Nimesema mara nyingi sana kwamba maneno Yangu lazima yatafakariwe kwa makini, na lazima yazingatiwe kwa makini. Je, kuna wowote kati yenu ambao ni watoto watiifu na wanyenyekevu? Je, Nimeongea bure? Je, hakuna matokeo kabisa? Ni kiasi gani cha yale yaliyo ndani yako yanayoweza kukidhi mapenzi Yangu? Iwapo, hata kama ni kwa muda mfupi, unashinda bila kukaripiwa, basi wewe utakuwa mpotovu na asiyedhibitika. Nisipoeleza wazi jinsi ya kutenda, au jinsi ya kuzungumza, je, inawezekana kwamba wewe huna wazo katika moyo wako? Nakwambia! Anayepata hasara ni yule ambaye ni mkaidi, ambaye hanyenyekei, ambaye anaamini kwa upofu! Kama mtu hawi makini kwa yale Ninayoyasema, kama hawezi kuelewa kila kitu, basi hataweza kuelewa nia Zangu, na hataweza kunitumikia Mimi. Mtu wa aina hii atashughulikiwa na Mimi, na atapambana na hukumu Yangu. Kutoelewa kila kitu ni kuwa fidhuli sana na kuwa na pupa kwa makusudi. Kwa hivyo Namchukia mtu wa aina hii, na Sina upole hata kidogo kwake, Simwonyeshi huruma yoyote ila uadhama wote na hukumu; ona kama bado unathubutu kunidanganya Mimi. Mimi ni Mungu ambaye huchunguza ndani kabisa ya moyo wa binadamu. Hoja hii yapaswa kuwa wazi kwa kila mtu; vinginevyo, wataendesha tu shughuli zao kwa njia ya kawaida na kunichukulia kwa njia isiyo ya dhati. Hii ndiyo sababu baadhi ya watu bila kujua hupigwa na Mimi. Nimesema kwamba Sitamshughulikia mtu yeyote pasi na haki, kwamba Sitafanya mambo mabaya, kwamba kila kitu Nifanyacho ni kwa mujibu wa mipango ya busara ya mkono Wangu.
Hukumu Yangu imeshuka juu ya watu wote wasionipenda kwa dhati, wakati ambapo itakuwa wazi ni nani Niliyemjaalia na kumchagua, na ni nani ambao wameondolewa na Mimi. Haya sharti yawekwe wazi moja baada ya jingine, bila kuficha chochote. Watu wote, matukio, na vitu vyote vinasimama na kuwepo ili kuleta maneno Yangu kwenye utimilifu, na yanajishughulisha katika kufanya kweli maneno yaliyonenwa na kinywa Changu. Dunia na miisho ya ulimwengu vyote vinadhibitiwa na Mimi pekee. Lazima Nimpige yeyote anayethubutu kutoyatii maneno Yangu au kukataa kuyafanya matendo Yangu kuwa sheria, nikimfanya mtu huyo azame kuzimuni na akome kuishi. Maneno Yangu yote yanafaa na sahihi bila uchafu wowote. Je, kuzungumza kwenu kunaweza kufanana na Kwangu? Yote ni marefu na ya kuchosha, hueleweki na huelezi kwa dhahiri, na bado unafikiri umepata baadhi ya mambo, kwamba uko karibu sana. Nakwambia! Jinsi mtu alivyo mwenye kiburi zaidi, ndivyo anavyokuwa mbali na viwango Vyangu. Haonyeshi kuzingatia mapenzi Yangu, naye hunidanganya Mimi na kuliaibisha jina Langu vikali zaidi! Huna haya! Huangalii kimo chako mwenyewe. Wewe ni mpumbavu na mjinga kiasi ulioje!
Maneno Yangu huonyesha mambo wakati wote na katika sehemu zote. Je, inaweza kuwa kwamba bado huelewi, na bado huna uhakika? Je, unataka kunisikitisha Mimi? Jikakamue, na utayarishe ujasiri wako. Simtendei kwa ubaya mtu yeyote ambaye ananipenda Mimi. Mimi huchunguza ndani kabisa ya moyo wa binadamu na Najua yote yaliyo katika moyo wa kila mtu. Haya yote yatadhihirishwa moja baada ya jingine, na yote yatapitia uchunguzi Wangu. Sitakosa kamwe kutotilia maanani mtu yeyote ambaye kwa kweli ananipenda Mimi. Wao wote ni wapokeaji wa baraka; wao ni kundi la wana wazaliwa wa kwanza ambao Nimewajaalia kuwa wafalme. Na kwa wale ambao hawanipendi Mimi kwa kweli, wao ni walengwa wa hila zao wenyewe, na ni wapokezi wa maafa, na pia imejaaliwa na Mimi. Usihangaike. Nitawafichua mmoja baada ya mwingine. Nimeitayarisha kazi hii mapema, na Nimeanza kufanya kazi hii. Yote ni ya utaratibu, sio machafuko hata kidogo. Tayari Nimemaliza kazi ya kuamua ni nani mteule na ni nani ameondolewa. Mmoja kwa mmoja watafichuliwa kwenu muone. Katika kipindi cha nyakati hizi mtaona kile mkono Wangu unachokifanya, watu wote wataona kwamba haki Yangu na uadhama Wangu haviruhusu kosa au upinzani kutoka kwa mtu yeyote, na kwamba mtu yeyote ambaye anakosea ataadhibiwa vikali.
Mimi Ndiye ambaye daima hukagua ndani kabisa ya moyo wa kila mtu. Msinione Mimi kutoka kwa nje tu. Wanadamu vipofu! Hamsikilizi maneno ambayo Nimeyazungumza wazi, na kabisa nyinyi hamniamini Mimi, ambaye ni Mungu Mwenyewe kamili. Bila shaka Sitamvumilia yeyote ambaye huthubutu kunirairai au kuficha chochote kutoka Kwangu.
Unakumbuka yale yote ambayo Nimesema? “Kuniona Mimi ni sawa na kuona kila moja ya siri iliyofichwa tangu milele hata milele.” Je, umeitafakari kwa makini kauli hii? Mimi ni Mungu. Siri Zangu zimeonyeshwa wazi kwa ajili yenu. Je, hamjaziona? Kwa nini hamnizingatii? Na mbona unamwabudu Mungu asiye yakini ambaye yuko katika mawazo yako? Ningewezaje Mimi—Mungu mmoja wa kweli—kufanya kosa lolote? Lione hili kwa udhahiri! Kuwa na uhakika kwalo! Kila neno Langu na amali, kila tendo Langu na kila mwendo, kutabasamu Kwangu, kula Kwangu, na mavazi Yangu, kila kitu Changu hufanywa na Mungu Mwenyewe. Mnanihukumu Mimi; je, yawezekana kuwa kwamba tayari mlimwona Mungu kabla ya ujio Wangu? Hivyo kwa nini siku zote wewe hunilinganisha Mimi na Mungu wako katika moyo wako? Zote ni dhana za wanadamu! Vitendo Vyangu na tabia haviambatani na mawazo yako, sivyo? Simruhusu mtu yeyote kutoa maoni kama vitendo Vyangu na tabia ni sahihi au la. Mimi ndiye Mungu mmoja wa kweli. Huu ni ukweli usiobadilika, na ulio sahihi kabisa! Usidanganywe na hila zako mwenyewe. Maneno Yangu yamesema kwa uwazi kabisa. Hakuna hata doa la ubinadamu ndani Yangu, na Mimi mzima ni Mungu Mwenyewe, aliyedhihirishwa kwenu kikamilifu, bila chochote kilichofichwa!