Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu katika Enzi ya Ufalme Wazitii
1. Mwanadamu hapaswi kujiinua, wala kujisifu. Anapaswa kumwabudu na kumsifu Mungu.
2. Unapaswa kufanya chochote ambacho kina manufaa kwa kazi ya Mungu, na hupaswi kufanya chochote ambacho kitaleta madhara kwa maslahi ya kazi ya Mungu. Unapaswa kulitetea jina la Mungu, ushuhuda Wake, na kazi ya Mungu.
3. Pesa, vitu vya dunia, na mali zote ambazo zipo katika nyumba ya Mungu ni sadaka ambazo zinapaswa kutolewa na mwanadamu. Sadaka hizi hazipaswi kufurahiwa na binadamu yeyote ila kuhani na Mungu Mwenyewe, kwani sadaka zinazotolewa na binadamu ni za kufurahiwa na Mungu, Mungu anashiriki tu sadaka hizi na kuhani, na hakuna mwingine yeyote aliyehitimu wala kuwa na haki ya kufurahia sehemu yoyote ya sadaka hizi. Sadaka zote zinazotolewa na mwanadamu (ikiwemo pesa, vifaa na vitu vinavyoweza kufurahiwa) vyote vinatolewa kwa Mungu, na sio kwa mwanadamu. Kwa hivyo, vitu hivi havipaswi kufurahiwa na mwanadamu; kama mwanadamu angekuwa anavifurahia vitu hivi, basi angekuwa anaiba sadaka. Yeyote yule atakayefanya hili ni msaliti kama Yuda, kwa kuwa, sio tu kwamba Yuda alikuwa msaliti, bali pia Yuda alijitwalia vilivyokuwa katika mfuko wa pesa ili kutumia.
4. Mwanadamu ana tabia potovu na, zaidi ya hayo, amejawa na hisia. Kwa hivyo, ni marufuku kabisa kwa watu wa jinsia mbili tofauti kufanya pamoja kazi wakati wa kumtumikia Mungu bila kuwepo na mtu mwingine. Yeyote yule atakayepatikana na kosa hili atafukuzwa, bila ubaguzi—na hakuna atakayeepuka hili.
5. Hupaswi kumhukumu Mungu, au kujadili kiholela mambo yanayomuhusu Mungu. Unapaswa kutenda vile mwanadamu anavyopaswa kutenda, na kuzungumza jinsi mwanadamu anavyopaswa kuzungumza, na hupaswi kuvuka upeo wako wala kuvuka mipaka yako. Uchunge ulimi wako na uwe mwangalifu kwa hatua zako. Yote haya yatakuzuia kufanya jambo lolote linaloweza kuikosea tabia ya Mungu.
6. Unapaswa kufanya yale yanayopaswa kufanywa na mwanadamu, na utekeleze wajibu wako, na utimize majukumu yako, na ushikilie wajibu wako. Kwa sababu unaamini katika Mungu, unapaswa kutoa mchango wako kwa kazi ya Mungu; kama huwezi, basi wewe hufai kula na kunywa maneno ya Mungu, na hufai kuishi katika nyumba ya Mungu.
7. Katika kazi na mambo yanayohusiana na kanisa, mbali na kumtii Mungu, katika kila kitu unapaswa kufuata maagizo ya mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu. Hata ukiukaji mdogo tu haukubaliki. Lazima uwe mkamilifu katika kutii kwako, na hupaswi kuchunguza kati ya mazuri na mabaya; yaliyo mazuri au mabaya hayakuhusu. Unapaswa kujishughulisha tu na utiifu kamili.
8. Watu wanaoamini katika Mungu wanapaswa kumtii na kumwabudu. Hupaswi kumsifu au kumwabudu mtu yeyote; hupaswi kumpa Mungu nafasi ya kwanza, binadamu unayemheshimu nafasi ya pili, kisha wewe mwenyewe nafasi ya tatu. Mtu yeyote asishikilie nafasi yoyote moyoni mwako, na hupaswi kuwachukulia watu—hasa wale unaowaheshimu—kuwa katika kiwango sawa na Mungu, kuwa sawa na Yeye. Mungu hawezi kustahimili hili.
9. Mawazo yako yanapaswa kuwa juu ya kazi ya kanisa. Unapaswa kuweka kando matarajio ya mwili wako, uwe na msimamo thabiti kuhusu mambo ya kifamilia, na ujitoe kwa moyo wako wote kwa kazi ya Mungu, na uiweke kazi ya Mungu kwanza kisha maisha yako katika nafasi ya pili. Huu ndio mwenendo mwema wa mtu mtakatifu.
10. Jamaa zako (watoto, mke au mume, dada zako au wazazi wako na kadhalika) wasio wa imani yako hawapaswi kulazimishwa kuja kanisani. Nyumba ya Mungu haina ukosefu wa washirika, na hakuna haja ya kuijaza na watu wasiokuwa na maana katika nyumba Yake. Wale wote wasioamini kwa moyo mchangamfu, hawapaswi kuongozwa kuingia kanisani. Amri hii inaelekezwa kwa watu wote. Kuhusu jambo hili mnapaswa kuchunguza, kufuatilia na kukumbushana, na hakuna anayepaswa kukiuka amri hii. Hata wakati jamaa zako wasio wa imani yako wanapoingia kanisani kwa i shingo upande, hawapaswi kupatiwa jina jipya wala kupewa vitabu vya kanisa; watu kama hao si wa nyumba ya Mungu, na kuingia kwao kanisani kunapaswa kukomeshwa kwa njia yoyote ile inayofaa. Ikiwa matatizo yataletwa kanisani kwa sababu ya uvamizi wa mapepo, basi wewe mwenyewe utafukuzwa au kuwekewa vikwazo. Kwa ufupi, kila mmoja ana jukumu katika suala hili, ingawa pia hupaswi kuwa mzembe, wala kutumia jambo hili ili kulipiza kisasi chako binafsi.