Waovu Hakika Wataadhibiwa

Jichunguzeni wenyewe ili mwone kama mnatenda haki katika mambo mnayofanya, na kama matendo yenu yanastahimili uchunguzi wa Mungu: Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo wale wanaomwamini Mungu huendesha mambo yao. Mtaitwa wenye haki kwa sababu mnaweza kumridhisha Mungu, na kwa sababu mnakubali utunzaji na ulinzi wa Mungu. Machoni pa Mungu, wale wote wanaokubali utunzaji, ulinzi, na kufanywa kuwa watimilifu na Mungu, na wanaopatwa na Yeye, ni watu wenye haki, na Yeye huwachukulia wote kuwa wa thamani. Kadiri mnavyokubali maneno ya sasa ya Mungu, ndivyo mtakavyoweza kuelewa na kufahamu nia za Mungu zaidi, na kwa hivyo ndivyo mtakavyoweza kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu na kukidhi matakwa Yake zaidi. Hili ni agizo la Mungu kwenu, na ndilo ambalo nyote mnapaswa kuweza kutimiza. Mkitumia mawazo yenu kumpima na kumwekea Mungu mipaka, kana kwamba Mungu ni sanamu ya udongo isiyobadilika, mkimwekea Mungu mipaka kabisa kwenye Biblia na kumweka Yeye ndani ya mawanda finyu ya kazi, basi hili linathibitisha kwamba mmemtia Mungu hatiani. Kwa sababu Wayahudi katika enzi ya Agano la Kale walimchukulia Mungu kuwa sanamu yenye umbo thabiti waliyoiweka mioyoni mwao, kana kwamba Mungu anaweza tu kuitwa Masihi, na ni Yeye tu aliyeitwa Masihi ndiye anayeweza kuwa Mungu, na kwa sababu watu walimtumikia na kumwabudu Mungu kana kwamba Yeye ni sanamu ya udongo (isiyo na uhai), walimsulubisha Yesu wa wakati huo msalabani, wakimhukumu kifo—Yesu asiye na hatia hivyo alihukumiwa kifo. Mungu hakuwa na hatia, lakini mwanadamu alikataa kumhurumia, na alisisitiza kumhukumu kifo, na hivyo Yesu alisulubiwa. Mwanadamu daima huamini kwamba Mungu habadiliki, na humwekea mipaka kwa msingi wa kitabu kimoja tu, Biblia, kana kwamba mwanadamu ana ufahamu kamili wa usimamizi wa Mungu, kana kwamba mwanadamu anashikilia yote anayofanya Mungu katika kiganja cha mkono wake. Watu ni wapuuzi kupindukia, wenye kiburi kupindukia, na wote wana mwelekeo wa kuzungumza maneno makubwa. Haijalishi maarifa yako kuhusu Mungu ni ya juu kiasi gani, bado Ninasema kwamba humjui Mungu, kwamba wewe ni mtu anayempinga Mungu zaidi ya wote, na kwamba umemtia Mungu hatiani, kwa sababu huwezi kabisa kutii kazi ya Mungu na kutembea katika njia ya kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu. Kwa nini Mungu haridhishwi kamwe na matendo ya mwanadamu? Ni kwa sababu mwanadamu hamjui Mungu kamwe, ana mawazo mengi mno, na maarifa yake kuhusu Mungu hayakubaliani na uhalisi kwa namna yoyote ile, bali ni ya kikanuni na ya kujirudiarudia, na yaliyonakiliwa kama mashine na kutumiwa bila kubadilika. Na hivyo, akiwa amekuja duniani leo, Mungu anasulubiwa msalabani kwa mara nyingine tena na mwanadamu. Mwanadamu mkatili! Hila na njama, kunyang'anyana na kupokonyana, kugombea umaarufu na faida, kuchinjana—je, yatakoma lini? Licha ya mamia ya maelfu ya maneno ambayo Mungu amenena, hakuna mtu ambaye amerudiwa na fahamu zake. Watu hutenda kwa ajili ya familia zao, wana na binti zao, kwa ajili ya taaluma zao, matarajio ya baadaye, hadhi, utukufu wa bure, na pesa, kwa ajili ya chakula, mavazi, na mwili. Lakini, je, kuna yeyote ambaye matendo yake ni kwa ajili ya Mungu kweli? Hata miongoni mwa wale wanaotenda kwa ajili ya Mungu, kuna wachache tu wanaomjua Mungu. Ni watu wangapi ambao hawatendi kwa ajili ya masilahi yao wenyewe? Ni wangapi ambao hawakandamizi au kuwatenga wengine ili kulinda hadhi yao wenyewe? Na hivyo, Mungu amehukumiwa kifo kwa nguvu mara zisizohesabika, na waamuzi wakatili wasiohesabika wamemtia Mungu hatiani na kumsulubisha msalabani kwa mara nyingine tena. Ni wangapi wanaoweza kuitwa watu wenye haki kwa sababu wanatenda kwa ajili ya Mungu kweli?

Je, ni rahisi sana kufanywa kuwa mtimilifu mbele za Mungu kuwa mtakatifu au mtu mwenye haki? Ni kauli ya kweli kwamba "hakuna wenye haki duniani humu, wenye haki hawako katika ulimwengu huu." Mnapokuja mbele za Mungu, fikirieni kile mnachovaa, fikirieni kila neno lenu, tendo lenu, na hatua yenu, kila wazo na fikira yenu, na hata ndoto mnazoota kila siku—yote ni kwa ajili yenu wenyewe. Je, hii si hali halisi ya mambo? "Haki" haimaanishi kuwapa wengine sadaka, haimaanishi kumpenda jirani yako kama unavyojipenda, na haimaanishi kujizuia na ugomvi na mizozo au kupora na kuiba. Haki inamaanisha kuchukua agizo la Mungu kama wajibu wenu na kutii mipango na mipangilio ya Mungu kama wito wenu uliotumwa kutoka mbinguni, bila kujali wakati au mahali, kama tu yote yaliyofanywa na Bwana Yesu. Hii ndiyo haki ambayo Mungu amezungumzia. Kwamba Lutu angeweza kuitwa mwenye haki ni kwa sababu aliwaokoa malaika wawili waliotumwa na Mungu bila kufikiria faida na hasara yake mwenyewe; inaweza tu kusemwa kwamba kile alichofanya wakati huo kinaweza kuitwa jambo la haki, lakini hawezi kuitwa mtu mwenye haki. Ilikuwa tu kwa sababu Lutu alikuwa amemwona Mungu ndiyo maana aliwatoa binti zake wawili badala ya malaika, lakini si tabia yake yote ya zamani iliwakilisha haki. Na hivyo Ninasema "hakuna wenye haki duniani humu." Miongoni mwa wale walio katika mkondo wa urejesho, hakuna anayeweza kuitwa mtu mwenye haki. Haijalishi matendo yako ni mazuri kiasi gani, haijalishi unaonekana kulitukuza jina la Mungu namna gani, bila kuwapiga na kuwalaani wengine, wala kuwapora na kuwanyang'anya wengine, bado huwezi kuitwa mwenye haki, kwani hiki ndicho ambacho mtu wa kawaida ana uwezo wa kuwa nacho. Kile ambacho ni muhimu sasa hivi ni kwamba humjui Mungu. Inaweza tu kusemwa kwamba kwa sasa una ubinadamu wa kawaida kiasi, lakini huna vipengele vya haki iliyozungumziwa na Mungu, na hivyo hakuna unachofanya ambacho kina uwezo wa kuthibitisha kwamba unamjua Mungu.

Hapo awali, Mungu alipokuwa mbinguni, watu walishughulika na Mungu kwa kijuujuu tu katika matendo yao. Leo, Mungu amekuwa miongoni mwa wanadamu kwa miaka isiyohesabika—na hakuna anayejua hili. Hata hivyo watu bado wanashughulika na Yeye kwa kijuujuu tu katika matendo yao. Je, watu hawako nyuma sana katika fikira zao? Wao ni kama Yuda tu: Kabla ya Yesu kuja, Yuda angesema uwongo ili kuwadanganya akina ndugu, na hata baada ya Yesu kuja, bado hakubadilika; hakumjua Yesu hata kidogo, na mwishowe alimsaliti Yesu. Je, hii haikuwa kwa sababu hakumjua Mungu? Ikiwa, leo, bado hamumjui Mungu, basi inawezekana kwamba mnaweza kuwa Yuda mwingine, na kufuatia hili, mkasa wa kusulubiwa kwa Yesu katika Enzi ya Neema miaka elfu mbili iliyopita unaweza kutokea tena. Je, hamwamini hili? Ni ukweli! Kwa sasa, watu wengi wako katika hali sawa na hii. Pengine ni mapema mno kusema hili, lakini watu kama hao wote wanachukua nafasi ya Yuda. Sizungumzi upuuzi, bali kwa msingi wa ukweli wa mambo—na huna budi kusadikishwa. Ingawa watu wengi hujifanya kuwa wanyenyekevu, mioyoni mwao hakuna chochote isipokuwa dimbwi la maji yaliyotuama, mtaro wa maji yanayonuka. Sasa hivi kuna wengi mno kama hawa kanisani, na mnafikiri kwamba sijui kuhusu hili kabisa. Leo, Roho Wangu ananitetea, na kunishuhudia. Je, unafikiri sijui chochote? Je, mnafikiri sielewi chochote kuhusu fikira potovu zilizo ndani ya mioyo yenu, mambo mnayoweka ndani ya mioyo yenu? Je, ni rahisi sana kumsumbua Mungu? Je, mnafikiri mnaweza kumtendea Yeye kwa njia yoyote mnayopenda? Zamani, Nilikuwa na wasiwasi msije mkabanwa, kwa hivyo Niliendelea kuwapa uhuru, lakini binadamu hakuthamini wema aliyoonyeshwa, na alipopewa nafasi kidogo, alienda zaidi ya alivyopewa. Ulizeni miongoni mwenu wenyewe: Karibu Sijawahi kumpogoa mtu yeyote, na karibu Sijawahi kumkemea mtu yeyote kwa wepesi—hata hivyo Ninaelewa waziwazi kuhusu motisha na mawazo ya mwanadamu. Je, unafikiri Mungu Mwenyewe, ambaye Mungu anamshuhudia, ni mpumbavu? Katika hali hiyo, Ninasema kwamba wewe ni kipofu mno! Sitakufichua, lakini tuone jinsi unavyoweza kuwa mpotovu. Tuone kama mbinu zako ndogo za ujanja zinaweza kukuokoa, au kama kujaribu kwako uwezavyo kumpenda Mungu kunaweza kukuokoa. Leo, Sitakutia hatiani; tusubiri hadi wakati wa Mungu ili kuona jinsi Anavyoleta adhabu juu yako. Sina muda wa kupiga soga na wewe sasa, na siko radhi kuchelewesha kazi Yangu kuu kwa ajili yako tu. Funza kama wewe hastahili muda ambao Mungu angechukua kukupogoa—kwa hivyo acha tuone jinsi unavyoweza kupotoka kabisa. Watu kama hawa hawafuatilii maarifa ya Mungu hata kidogo, wala hawana hata chembe ya moyo umpendao Mungu, na bado wanatamani Mungu awaite watu wenye haki—je, huu si utani? Kwa sababu idadi ndogo ya watu ni waaminifu kwa kweli, Nitalenga tu kuendelea kumpa mwanadamu uzima. Nitafanya tu kile Ninachopaswa kufanya leo, lakini katika siku za usoni Nitaleta adhabu juu ya kila mtu kulingana na kile ambacho amefanya. Nimesema yote yanayopasa kusemwa, kwani hii hasa ndiyo kazi Ninayofanya. Ninafanya tu kile Ninachopaswa kufanya, na si kile Nisichopaswa kufanya. Hata hivyo, Ninatumai kwamba mnajichunguza zaidi: Ni kiasi gani cha maarifa yako kuhusu Mungu ni cha kweli hasa? Je, wewe ni mtu ambaye amemsulubisha Mungu msalabani kwa mara nyingine tena? Maneno Yangu ya mwisho ni haya: Ole wao wanaomsulubisha Mungu.

Iliyotangulia:  Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Inayofuata:  Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Connect with us on Messenger