Unapaswa Kujua Kwamba Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe
Unapaswa kujua nini kuhusu Mungu wa vitendo? Roho, Nafsi, na Neno ndivyo vinajumuisha Mungu wa vitendo Mwenyewe, na hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu wa vitendo Mwenyewe. Ikiwa unaijua Nafsi pekee—ikiwa unajua tabia Zake za kila siku na sifa Zake bainifu—lakini hujui kazi ya Roho, au kile ambacho Roho anafanya katika mwili, na ukizingatia tu Roho, na Neno, na kuomba tu mbele ya Roho, lakini hujui kazi ya Roho wa Mungu katika Mungu wa vitendo, basi hili bado linathibitisha kwamba humjui Mungu wa vitendo. Ujuzi wa Mungu wa vitendo unajumuisha kuyajua na kuyapitia maneno Yake, na kufahamu sheria na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu na jinsi Roho wa Mungu anavyofanya kazi katika mwili. Pia unajumuisha kujua kwamba kila kitendo cha Mungu katika mwili kinaelekezwa na Roho, na kwamba maneno Anayozungumza ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Hivyo, ili kumjua Mungu wa vitendo, ni jambo lenye umuhimu mkubwa kujua jinsi Mungu anavyofanya kazi katika ubinadamu na katika uungu; hili, kwa upande mwingine, linahusu maonyesho ya Roho, ambayo watu wote wanajihusisha nayo.
Vipengele vya maonyesho ya Roho ni vipi? Wakati mwingine Mungu anafanya kazi katika ubinadamu, na wakati mwingine katika uungu—lakini katika hali zote mbili Roho ndiye anayeongoza. Maonyesho ya nje ya Nafsi yanategemea Roho aliye ndani Yake. Roho anafanya kazi kwa kawaida, lakini kuna sehemu mbili za maelekezo Anayopewa na Roho: Sehemu moja ni kazi Yake katika ubinadamu, na nyingine ni kazi Yake kupitia uungu. Unapaswa kujua hili waziwazi. Kazi ya Roho inatofautiana kulingana na hali: Wakati ubinadamu Wake unahitajika kufanya kazi, Roho anaelekeza ubinadamu huu kufanya kazi hii, na wakati uungu Wake unahitajika kufanya kazi, uungu unajitokeza moja kwa moja kuitekeleza. Kwa sababu Mungu anafanya kazi katika mwili na anaonekana katika mwili, Yeye anafanya kazi katika ubinadamu na katika uungu. Kazi Yake katika ubinadamu inaelekezwa na Roho na inafanywa ili kukidhi mahitaji ya kimwili ya watu, kuwezesha kujihusisha kwao na Yeye, kuwaruhusu waone uhakika na ukawaida wa Mungu, na kuwaruhusu waone kwamba Roho wa Mungu amekuja katika mwili na yuko miongoni mwa wanadamu, anaishi pamoja na wanadamu, na anajihusisha na wanadamu. Kazi Yake katika uungu inafanywa ili kuruzuku maisha ya watu na kuwaongoza watu katika kila kitu kutoka upande chanya, ikibadilisha tabia za watu na kuwaruhusu waone kwa kweli kuonekana kwa Roho katika mwili. Kimsingi, ukuaji katika maisha ya mwanadamu unafikiwa moja kwa moja kupitia kazi na maneno ya Mungu katika uungu. Watu wakiikubali kazi ya Mungu katika uungu tu ndipo wanaweza kufikia mabadiliko katika tabia zao, na ni hapo tu ndipo wanaweza kushibishwa katika roho zao; ni ikiwa tu, kuongeza kwa hili, kuna kazi katika ubinadamu—uchungaji, utegemezo, na ruzuku ya Mungu katika ubinadamu—ndipo matokeo ya kazi ya Mungu yanaweza kufikiwa kikamilifu. Mungu wa vitendo Mwenyewe anayezungumziwa leo anafanya kazi katika ubinadamu na katika uungu. Kupitia kuonekana kwa Mungu wa vitendo, kazi na maisha Yake ya kawaida ya kibinadamu na kazi Yake ya uungu kamili vinafikiwa. Ubinadamu na uungu Wake vimeunganishwa kuwa kimoja, na kazi ya vyote viwili inakamilishwa kupitia maneno; iwe katika ubinadamu au uungu, Yeye anatamka maneno. Mungu anapofanya kazi katika ubinadamu, Yeye anazungumza lugha ya ubinadamu, ili watu waweze kujihusisha nayo na kuelewa kwa urahisi zaidi. Maneno Yake yanazungumzwa waziwazi na ni rahisi kuelewa, kiasi kwamba yanaweza kutolewa kwa watu wote; bila kujali kama watu wana maarifa au wana elimu duni, wote wanaweza kupokea maneno ya Mungu. Kazi ya Mungu katika uungu pia inatekelezwa kupitia maneno, lakini imejaa ruzuku, imejaa uzima, haijachafuliwa na mawazo ya binadamu, haihusishi mapendeleo ya binadamu, na haiko chini ya mipaka ya binadamu, haifungwi na vizuizi vyovyote vya ubinadamu wa kawaida; pia inatekelezwa katika mwili, lakini ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho. Watu wakikubali tu kazi ya Mungu katika ubinadamu, basi watajifungia katika upeo fulani, na hivyo watahitaji upogoaji na kutiwa adabu kwa kudumu ili kuwe na hata mabadiliko kiasi kidogo ndani yao. Hata hivyo, bila kazi au uwepo wa Roho Mtakatifu, daima watakimbilia njia zao za zamani. Ni kupitia kazi ya uungu ndiyo kasoro hii na upungufu huu unafidiwa, na watu kufanywa kuwa kamili. Badala ya upogoaji endelevu, kinachohitajika ni ruzuku chanya, kutumia maneno kufidia mapungufu yote, kutumia maneno kufunua kila hali ya watu, kutumia maneno kuelekeza maisha yao, kila tamko lao, kila kitendo chao, kuweka wazi nia na misukumo yao. Hii ndiyo kazi ya vitendo ya Mungu wa vitendo. Hivyo, katika mtazamo wako kwa Mungu wa vitendo, unapaswa kutii mbele ya ubinadamu Wake, kumtambua na kumkiri Yeye, na zaidi sana unapaswa kukubali na kutii kazi Yake na maneno Yake katika uungu. Kuonekana kwa Mungu katika mwili kunamaanisha kwamba kazi yote na maneno yote ya Roho wa Mungu yanafanywa kupitia ubinadamu Wake wa kawaida na kupitia mwili Wake. Kwa maneno mengine, Roho wa Mungu anauelekeza ubinadamu Wake mara moja kufanya kazi, na anatekeleza kazi ya uungu katika mwili, na katika Mungu mwenye mwili unaweza kuona kazi ya Mungu katika ubinadamu na kazi Yake katika uungu kamili. Huu ndio umuhimu halisi wa kuonekana kwa Mungu wa vitendo katika mwili. Ikiwa unaweza kuona hili waziwazi, utaweza kuunganisha sehemu zote tofauti za Mungu; utaacha kutilia maanani kupita kiasi kazi Yake katika uungu, na utaacha kuichukulia kazi Yake katika ubinadamu kwa dharau kupita kiasi, na hutazidi kiasi, wala kuchukua njia zozote za mchepuko. Kwa ujumla, maana ya Mungu wa vitendo ni kwamba kazi ya ubinadamu Wake na ya uungu Wake, kama inavyoelekezwa na Roho, inaonyeshwa kupitia mwili Wake, ili watu waweze kuona kwamba Yeye ni mwenye uhai na hai, halisi na wa kweli.
Kazi ya Roho wa Mungu katika ubinadamu ina awamu ya mpito. Kwa kufanya ubinadamu kuwa timilifu, Yeye huwezesha ubinadamu Wake kupokea maelekezo ya Roho, na baada ya hapo ubinadamu Wake unaweza kuruzuku na kuyachunga makanisa. Hili ni onyesho moja la kazi ya kawaida ya Mungu. Hivyo, ikiwa unaweza kuona waziwazi kanuni za kazi ya Mungu katika ubinadamu, basi huenda usiwe na dhana kuhusu kazi ya Mungu katika ubinadamu. Bila kujali chochote kingine, Roho wa Mungu hawezi kukosea. Yeye yuko sahihi na hana kosa; Yeye hafanyi chochote kimakosa. Kazi katika uungu ni maonyesho ya moja kwa moja ya nia za Mungu, bila usumbufu wa ubinadamu. Haipitii kufanywa kuwa timilifu, bali inatoka moja kwa moja kwa Roho. Hata hivyo, hata Anapofanya kazi katika uungu, pia ni kwa sababu ya ubinadamu Wake wa kawaida; si ya kimuujiza hata kidogo, na inaonekana kutekelezwa na mtu wa kawaida. Mungu alikuja kutoka mbinguni hadi duniani kimsingi ili kuonyesha maneno ya Mungu kupitia mwili—kukamilisha kazi ya Roho wa Mungu kwa njia ya mwili.
Leo, maarifa ya watu kuhusu Mungu wa vitendo yanabaki kuwa ya upande mmoja mno, na uelewa wao wa umuhimu wa kupata mwili bado ni duni sana. Kuhusiana na mwili wa Mungu, watu wanaona kupitia kazi na maneno Yake kwamba Roho wa Mungu anajumuisha mengi sana, kwamba Yeye ni tajiri sana. Hata hivyo, haijalishi chochote, ushuhuda wa Mungu hatimaye unatokana na Roho wa Mungu: kile ambacho Mungu anafanya katika mwili, kanuni ambazo kwazo Yeye anafanya kazi, kile Anachofanya katika ubinadamu, na kile Anachofanya katika uungu. Watu lazima wawe na maarifa ya hili. Leo, unaweza kuiabudu Nafsi hii, huku kimsingi unamwabudu Roho, na hilo ndilo jambo la kiwango cha chini kabisa ambalo watu wanapaswa kufikia katika maarifa yao ya Mungu mwenye mwili. Kwa njia ya mwili, watu wanafikia kujua kiini cha Roho, kujua kazi ya kiungu ya Roho katika mwili na kazi ya binadamu katika mwili, kukubali maneno na matamko yote ya Roho katika mwili, na kuona jinsi Roho wa Mungu anavyoelekeza mwili na kufunua nguvu Zake katika mwili. Hili ni kusema kwamba mwanadamu anafikia kumjua Roho mbinguni kupitia mwili; kuonekana kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe miongoni mwa wanadamu kumetawanya mungu asiye yakini aliye katika dhana za watu. Ibada ya watu kwa Mungu wa vitendo Mwenyewe imeongeza utii wao kwa Mungu, na, kupitia kazi ya kiungu ya Roho wa Mungu katika mwili na kazi Yake ya kibinadamu katika mwili, mwanadamu anapokea ufunuo na anachungwa, na mabadiliko yanafikiwa katika tabia ya maisha ya mwanadamu. Hii ndiyo maana halisi ya kuwasili kwa Roho katika mwili, ambako dhumuni lake kuu ni kwamba watu waweze kujihusisha na Mungu, kumtegemea Mungu, na kufikia maarifa ya Mungu.
Kimsingi, watu wana mtazamo gani kwa Mungu wa vitendo? Unajua nini kuhusu kupata mwili, kuhusu kuonekana kwa Neno katika mwili, kuhusu kuonekana kwa Mungu katika mwili, kuhusu matendo ya Mungu wa vitendo? Mada kuu za majadiliano leo ni zipi? Kupata mwili, kuwasili kwa Neno katika mwili, na kuonekana kwa Mungu katika mwili yote ni masuala ambayo lazima yaeleweke. Mnapaswa kufikia hatua ya kuelewa masuala haya polepole na kuwa na maarifa dhahiri kuyahusu katika upitiaji wenu wa maisha, kulingana na kimo chenu na kulingana na enzi. Mchakato wa watu kupitia maneno ya Mungu ni mchakato wao wa kufikia kujua kuonekana kwa maneno ya Mungu katika mwili. Kadiri watu wanavyopitia maneno ya Mungu zaidi, ndivyo wanavyomjua Roho wa Mungu zaidi; kwa kupitia maneno ya Mungu, watu wanafahamu kanuni za kazi ya Roho na kufikia kumjua Mungu wa vitendo Mwenyewe. Kwa kweli, Mungu anapowafanya watu kuwa watimilifu na kuwapata, Yeye anawajulisha matendo ya Mungu wa vitendo; Yeye anatumia kazi ya Mungu wa vitendo kuwaonyesha watu umuhimu halisi wa kupata mwili, kuwaonyesha kwamba Roho wa Mungu ameonekana kwa kweli mbele ya mwanadamu. Watu wanapopatwa na kufanywa kuwa watimilifu na Mungu, hii inamaanisha kwamba maonyesho ya Mungu wa vitendo yamewashinda, na kwamba—kwa njia ya maneno ya Mungu wa vitendo—wamebadilishwa, na maisha Yake yamefinyangwa ndani yao, yakiwajaza na kile Alicho (iwe ni kile Alicho katika ubinadamu Wake au kile Alicho katika uungu Wake), yakiwajaza na kiini cha maneno Yake, na kuwafanya watu waishi kwa kudhihirisha maneno Yake. Mungu anapowapata watu, Yeye hufanya hivyo kimsingi kwa kutumia maneno na matamko ya Mungu wa vitendo kama njia ya kupogoa mapungufu ya watu na kuhukumu na kufichua tabia yao ya uasi, na kuwafanya wapate kile wanachohitaji na kuwaonyesha kwamba Mungu amekuja miongoni mwa wanadamu. Muhimu zaidi ya yote, kazi inayofanywa na Mungu wa vitendo ni ile ya kumwokoa kila mtu kutoka katika ushawishi wa Shetani, kuwatoa kutoka katika nchi ya uchafu, na kung'oa tabia zao potovu. Umuhimu wa kina zaidi wa kupatwa na Mungu wa vitendo ni kuweza kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida huku Mungu wa vitendo akiwa sampuli na mfano, na kuweza kutenda kulingana na maneno na matakwa ya Mungu wa vitendo bila ukengefu au mkengeuko hata kidogo, kutenda kulingana na chochote Anachosema, na kuweza kufikia chochote Anachotaka. Kwa njia hii, utakuwa umepatwa na Mungu. Unapopatwa na Mungu, humiliki tu kazi ya Roho Mtakatifu; kimsingi, unaweza kuishi kwa kudhihirisha matakwa ya Mungu wa vitendo. Kuwa tu na kazi ya Roho Mtakatifu hakumaanishi kwamba una uzima. Jambo la msingi ni iwapo unaweza kutenda kulingana na matakwa ya Mungu wa vitendo kwako, jambo ambalo linahusiana na iwapo unaweza kupatwa na Mungu. Hizi ndizo maana kuu zaidi za kazi ya Mungu wa vitendo katika mwili. Hili ni kusema, Mungu kwa kweli na kwa uhakika anaonekana katika mwili—mwenye uhai na hai—akiwaruhusu watu wamwone Yeye, na anatekeleza kwa njia ya vitendo kazi ya Roho katika mwili, na anatenda kama sampuli kwa watu katika mwili, ambao kwao Yeye anapata kikundi cha watu. Kuwasili kwa Mungu katika mwili kimsingi kunakusudiwa kuwawezesha watu kuona matendo ya vitendo ya Mungu, na kumfanya Roho asiye na umbo kuwa dhahiri katika mwili ili watu waweze kumwona na kumgusa Yeye. Ni kwa njia hii tu ndiyo wale wanaofanywa kuwa kamili na Yeye wataishi kwa kudhihirisha kile Anachoishi kwa kudhihirisha, watapatwa na Yeye, na watalingana na nia Zake. Mungu angezungumza tu mbinguni na asingekuja duniani kwa kweli, basi watu bado wasingeweza kumjua Mungu; wangeweza tu kuhubiri matendo ya Mungu wakitumia nadharia tupu na wasingekuwa na maneno ya Mungu kama uhalisi. Dhumuni la Mungu katika kuja duniani kimsingi ni kujiweka Mwenyewe kama sampuli na mfano kwa wale ambao Yeye atawapata; ni kwa njia hii tu ndiyo watu wanaweza kumjua Mungu kwa kweli, kumgusa Mungu, na kumwona Yeye, na ni hapo tu ndipo wanaweza kupatwa na Mungu kwa kweli.